Kinga Madhubuti Dhidi Ya COVID19
- Mwili unapoambukizwa na virusi🦠🦠vya COVID19, mfumo wake wa kinga (Immunity System)huanza kutengeneza kingamwili (antibodies)ambazo huwa na uwezo wa kutambua na kupambana na virusi 🦠🦠🦠na hatimae kinga ya mwili ikiwa imara virusi 🦠🦠hivi kuondolewa mwilini kabisa.
- Mtu akipona maana yake ameweza kutengeneza kingamwili (Antibodies)za kutosha zilizofanikiwa kuondoa virusi 🦠🦠vyote.
- Licha hivyo kinga ya mwili (immunity system)pia hutengeneza seli za kumbukumbu(memory cells) kwa ajili ya kuukumbusha mwili endapo maambukizi yatajitokeza kwa mara nyingine.
- Hivyo basi kuna uwezekano wa kuchukua Utegili (plasma)kutoka kwenye damu ya watu waliopona ambayo huwa na kingamwili(antibodies) dhidi ya virusi🦠🦠vya COVID19kuwapatia wagonjwa mahututi wa Corona ili kusaidia wapate kinga itakayosaidia kuviondoa virusi🦠🦠ndani ya miili yao.
- Kitendo hiki pia kinaweza kufanywa kwa watu wasio na maambukizi ya COVID19 ili kuwezesha wili kutengeneza kinga ya pili (secondary immunity)
- Tiba hii inaitwa Convalescent Plasma Therapy, ni tiba ya muda mrefu na matabibu wameitumia kwa muda mrefu.
- Tiba hii imesaidia sana kwenye magonjwa yatokanayo na virusi yaliyokuwa hayana dawa wala chanjo kama vile Surua(Measles), Ebola, SARS(Severe Acute Respiratory Syndrome) pamoja na mlipuko wa mafua ya HISPANIA.
- https://www.jwatch.org/na51335/2020/04/16/convalescent-plasma-therapy-patients-with-severe-covid-19


